MTANGAZAJI

UTAFITI - UMUHIMU WA MIKUTANO YA DINI KWA VIJANA

 


Utafiti mpya kutoka Chuo Kikuu cha Georgia (UGA) Marekani umesisitiza kuwa jukumu muhimu ambalo mikusanyiko inayohusisha jumuiya za imani dhabiti huchukua  nafasi katika kusaidia ukuaji wa kiroho wa vijana.

Hatua imeonyesha pia kwamba hisia ya kuwahusisha vijana  inaweza kuwa na jukumu muhimu katika kusaidia kuamua kama wataendelea na safari yao ya imani wanapokuwa wakubwa badala ya kupeperushwa mbali na kanisa.

Bill Stanford, mwandishi mkuu wa utafiti na mhitimu wa udaktari katika Chuo cha Familia na Sayansi ya huduma ya Chuo Kikuu cha Georgia anaeleza kuwa "Ilikuwa dhana tu kwamba watu wanaacha kuhudhuria ibada chuoni na kisha wakarudi wakiwa na watoto ,Lakini tafiti za hivi karibuni zaidi zimeonyesha kuwa watu hawarudi baada ya kupata watoto."

Katika mahojiano yaliyochukua miaka kadhaa ikiwa ni sehemu ya Utafiti wa Kitaifa wa Vijana na Dini, watafiti walikusanya majibu kutoka kwa zaidi ya vijana 1,700 na walezi wao, na kuunda picha ya kina ya mawazo na hisia zao kuhusu dini na kiroho.

Utafiti huo uligundua kwamba ingawa wazazi wanabaki kuwa ushawishi mkubwa katika kuendeleza imani kwa watoto, mikutano ya ibada inajukumu muhimu.

Pia  uligundua kuwa vijana walioshiriki katika vikundi vya vijana na elimu ya kidini, na ambao walihudhuria makanisa ambapo walitarajiwa kuhudhuria ibada mara kwa mara, walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuripoti viwango vya juu vya mazoezi ya kibinafsi ya kidini.

Ingawa zaidi ya robo tatu ya wazazi waliohojiwa walisema kwamba imani yao ilikuwa na fungu muhimu katika maisha yao ya kila siku na mchakato wa kufanya maamuzi, huku zaidi ya nusu wakihudhuria kanisa kila juma, chini ya nusu ya watoto wao walisema kwamba walijadili dini na wazazi wao mara kwa mara wengine wakisema kuwa hawajawahi kufanya hivyo.

Ted Futris, mwandishi mwenza wa utafiti huo na profesa wa maendeleo ya binadamu na sayansi ya familia, aliiambia UGA Today kwamba kuelimisha wazazi kuhusu jinsi ya kushughulikia mambo ya kiroho na watoto wao kunahitaji kujadiliwa zaidi.

Huku idadi ya watu wanaojitambulisha kuwa wasio na dini ikiendelea kukua, watafiti wanaamini kuwa kuhakikisha vijana wanatiwa moyo katika imani yao kupitia jumuiya zao ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.










No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.