MTANGAZAJI

MAKANISA YA ANGLIKANA UINGEREZA KUKODISHWA

 


Ili kukabiliana na kupungua kwa mahudhurio ya kawaida ya ibada, Kanisa la Anglikana nchini Uingereza  limependekeza mpango wa kukodisha makanisa ya Parokia ambayo hayatumiki sana badala ya kuyauza, na kuyapa na uwezekano wa kufunguliwa tena siku zijazo.

Pendekezo hilo linakuja kujibu mazoea ya sasa ya kuunganisha makanisa ambayo hayahudhuriwi vizuri na parokia kubwa na kuuza majengo yaliyoachwa.

Mpango huo, unaozingatiwa na Sinodi Kuu ambacho ni chombo cha kutunga sheria cha Kanisa hilo nchini Uingereza unapendekeza suluhisho ambalo linalenga kuhifadhi majengo hayo, kuyakodisha kwa mamlaka za mitaa, madhehebu mengine ya Kikristo, au taasisi nyingine chini ya mikataba ya umiliki wa pamoja.

Makamishna wa Kanisa la Uingereza, kundi linalohusika na kusimamia hazina ya ya Kanisa hilo yenye thamani ya dola bilioni 13 na walipendekeza mpango huo.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Telegram linaonesha kuwa Makanisa ya Anglikana nchini Uingereza yapatayo 423 yamefungwa kati ya 2010 na 2019, na karibu makanisa 1,000 yamefungwa kutoka 1987 hadi 2019. Kupungua huku kumefanya idadi ya makanisa yanayofanya kazi hadi karibu 15,496.

Wakati huo huo, sehemu ya jumla ya Ukristo ya idadi ya watu nchini Uingereza na Wales imeshuka. Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu za Kitaifa, Wakristo walikuwa 46.2% ya idadi ya watu mnamo 2021, kupungua kutoka 59.3% mnamo mwaka  2011.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.