MTANGAZAJI

UTAFITI : ASILIMIA KUBWA YA WAMAREKANI HAWAKUBALI MABADILIKO YA JINSIA

 


Kuzuia haki za waliobadili jinsia kumekuwa kilio cha hadhara kwa makundi ya watu  na sehemu ya wahafidhina wa kidini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita nchini Marekani na uchunguzi mpya unaonyesha kuwa kuna athari zake.

Uchunguzi wa Taasisi ya Utafiti wa Dini ya Umma (PRRI)  kwa  Wamarekani 5,438 unaonyesha ongezeko katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa imani kwamba kuna vitambulisho viwili tu vya kijinsia - mwanamume na mwanamke - kati ya vikundi kadhaa vya kidini.

Kwa makisio inaonekana kuwa, wainjilisti wa kizungu ambao data zinaonyesha kushikilia imani kali za kihafidhina walikua thabiti zaidi juu ya suala hilo katika miaka miwili iliyopita; 92% walisema kuna jinsia mbili tu, kutoka 86% ya mwaka 2021.

Lakini wengi wa vikundi vingine vya kidini pia hawakubali utambulisho wa kubadili jinsia

Wakatoliki Wahispania waliongoza msimamo huo. Utafiti unaonyesha 66% ya Wakatoliki wa Kihispania waishio Marekani  wanaamini kuna jinsia mbili tu - kutoka 48% mnamo 2021.

Wengi wa Wamarekani wengine wasio Wakristo, wakiwemo Waislamu, Wabudha, Wahindu na hata wasiotambua dini zao  pia wanasema kuna jinsia mbili tu.

Takriban 65% ya Wamarekani kwa ujumla, kutoka 59% miaka miwili iliyopita, wanasema kuna jinsia mbili tu.

Melissa Deckman Mtendaji mkuu wa PRRI anasema wanaona ugumu wa maoni kuhusu mfumo wa kijinsia katika makundi mengi na watu wa imani na bado ni wazo ambalo ni geni sana kwa watu wengi, haswa Wamarekani wazee, ambao huwa watu wa imani.

Zaidi ya miswada 500 dhidi ya LGBTQ imewasilishwa katika mabunge ya majimbo nchini Marekani mwaka huu.

Takriban miswada  80 imepita. Majimbo kumi na tisa sasa yana sheria zinazozuia ubadilishaji wa  jinsia ikiwemo  vizuizi vya kubalehe, tiba ya uingizwaji wa homoni na upasuaji kwa vijana walio na mabadiliko makubwa ya jinsia.
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.