MKE WA MCHUNGAJI AFUNGUA KESI DHIDI YA MALAYSIA
Mke wa Mchungaji aliyetekwa nyara mwaka 2017 ameanza kesi ya madai dhidi ya serikali ya Malaysia na Jeshi la polisi kwa lengo la kufichua ukweli.
Mchungaji Raymond Koh hajaonekana tangu alipotekwa nyara mchana kweupe Februari 2017 na kundi la washambuliaji 15 waliojifunika nyuso zao wakiwa kwenye gari zenye muundo SUV zilizokuwa zimezimwa. Walizunguka gari lake kabla ya kuondoka naye.
Kufuatia uchunguzi, Tume ya Haki za Binadamu ya Malaysia (SUHAKAM) ilihitimisha mnamo 2019 kwamba Koh alikuwa ametekwa nyara na Tawi Maalum la Idara ya Polisi ya Malaysia.
Serikali kisha ilizindua kikosi kazi cha uchunguzi wa tukio hilo na ilitakiwa kutoa matokeo hayo mwaka wa 2019 lakini ripoti hiyo haijawahi kuchapishwa.
Mkewe, Susanna Koh, anaamini kwamba serikali na polisi wanaficha ukweli kuhusu kilichompata.
Ikiwa ni sehemu ya kesi yake ya madai, anataka serikali ichapishe matokeo yake kuhusu kutoweka kwake.
Usikilizaji wa kwanza wa kesi yake ya madai ulifanyika katika Mahakama Kuu juma lililopita na ulijumuisha ushahidi kutoka kwa mashahidi wa utekaji nyara huo.
Familia ya Koh inaamini kuwa kutekwa nyara kwake kunahusishwa na kazi yake na shirika lake la hisani la Harapan Komuni linalomaanisha Jumuiya ya Matumaini ambalo inafanya kazi ya kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya, watu wasio na makazi, wazazi wasio na wenzi, na watu wenye VVU na UKIMWI.
Susanna Koh anasema Kulikuwa na madai kwamba alikuwa akibadilisha Waislamu kupitia shirika hilo lakini hakuna ushahidi wowote.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu juni 20 mwaka huu.
Post a Comment