MTANGAZAJI

MAHUBIRI NA MUZIKI WA KIPROTESTANTI WAWAVUTIA WENGI MAREKANI

 


Makanisa ya Kiprotestanti nchini Marekani yanaonekana kujivunia mahubiri na muziki wao tofauti makanisa  yanayotegemea Biblia pekee katika  ibada zao.Ambapo kwa kwa upande mwingine wa wigo ni makanisa ya Kikatoliki, ambayo yanaelezwa kuwa  mapokeo ya  mahubiri na muziki usiopendwa  zaidi nchini humo.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanya na Kituo cha Utafiti cha Pew kutokana na maoni ya Wakatoliki wenyewe. Pew haikupanga kufanya tathmini hii makusudi.
Ilitokana na utafiti, uliofanywa mnamo Novemba mwaka jana na kutolewa mapema mwezi huu, ukihusisha  na mahudhurio ya ibada mtandaoni na ana kwa ana kanisani.
Walichogundua ni kwamba Waprotestanti wanaridhika zaidi na mahubiri na muziki wao kuliko Wakatoliki.
Utafiti wa Pew unaonesha kuwa Watu wazima wa  Marekani walipoulizwa jinsi walivyoridhishwa na mahubiri waliyosikia mtandaoni au ana kwa ana, 82% ya Waprotestanti ambao walihudhuria ibada mara kwa mara walisema kwamba waliridhika sana na mahubiri wanayosikia.
Kwa Waprotestanti ambao walitazama huduma hyo  mara kwa mara kwenye TV au mtandaoni, 76% waliridhika sana na  mahubiri.
Kwa upande mwingine, ni 61% tu ya Wakatoliki nchini Marekani wanaohudhuria kanisa mara kwa mara ama ana kwa ana walisema walikuwa wameridhika sana , tofauti ya pointi 21 kutoka kwa Waprotestanti. Vile vile, kati ya Wakatoliki ambao hutazama huduma ya Ibada mara kwa mara kwenye TV au mtandaoni, 57% waliridhika sana ikiwa ni tofauti ya pointi 19.
Inaelezwa kuwa Kwa Wakatoliki, kiini cha ibada yao  kimekuwa ni huduma ya  Ekaristi, na si Neno.
Kwa mujibu wa Pew ni 36% tu ya Wakatoliki wanaosoma Maandiko ya Biblia  mara moja kwa mwezi au zaidi, ikilinganishwa na 75% ya Waprotestanti.
Miongoni mwa Waprotestanti, 75% ya wale wanaohudhuria huduma za Ibada  mara kwa mara  na ana kwa ana na 57% ya wale wanaotazama mara kwa mara kwenye TV au mtandaoni wanaridhika sana na muziki wao. Kwa Wakatoliki, idadi sawa ni 61% na 50%.
Takriban mtu 1 kati ya 3 nchini Marekani  waliolelewa katika Kanisa Katoliki wameacha Kanisa hilo kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew mwaka wa 2011. Takriban nusu yao wanakuwa Waprotestanti na nusu yao hawana makanisa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.