MTANGAZAJI

ADHANA KWA UMMA YARUHUSIWA KATIKA JIJI LA MINNEAPOLIS

 


Jiji la Minneapolis nchini Marekani limeruhusu matangazo ya mwito maalum wa kuwaita  Waislamu kwenda kusali saa zote, na kuwa jiji la kwanza kuu la Marekani kuruhusu tangazo la  "adhana" kusikika mara tano kwa siku kwa umma kwa kipindi cha mwaka mzima.

Halmashauri ya Jiji la Minneapolis ilikubali kwa kauli moja Aprili 13 mwaka huu kurekebisha sheria ya kelele katika jiji hilo, ambayo ilikuwa imezuia kusikika kwa adhana  alfajiri na jioni wakati fulani wa mwaka kwa sababu ya vizuizi vya kelele.

Kura hiyo imefayika wakati wa mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani.

"Minneapolis imekuwa jiji la dini zote," amesema Imam Mohammed Dukuly wa Msikiti wa Masjid An-Nur huko Minneapolis, ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi kadhaa wa Kiislamu walioshuhudia kura hiyo.

Minneapolis imekuwa na idadi kubwa ya wahamiaji wa Afrika Mashariki tangu  mwaka 1990, na misikiti sasa ni ya kawaida kwenye jiji hilo ambapo Wajumbe watatu kati ya 13 wa baraza hilo wanajitambulisha kuwa Waislamu. Uamuzi huo haukuleta upinzani uliopangwa wa jamii.

Meya wa Minneapolis Jacob Frey anatarajiwa ametiasaini hatua hiyo jumahili.

Mjumbe wa Baraza Lisa Goodman, ambaye Alhamisi alikuwa akiadhimisha siku ya mwisho ya Pasaka, alisema mwito wa Wayahudi kwa maombi - ambao huzungumzwa kwa ujumla badala ya kutangazwa - haukabiliani na vizuizi vya kisheria.Huku waangalizi wakieleza kuwa kengele za kanisa hulia mara kwa mara kwa Wakristo.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.