MTANGAZAJI

WAKAAZI WAMTETEA MCHUNGAJI MWENYE TUHUMA

 


Wakaazi wa kisiwa cha Ngodhe kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wamejitokeza kumtetea vikali Mchungaji Ezekiel Ombok Odero wa kanisa la New Life Prayer Centre ambaye kwa sasa anazuiliwa na polisi kufuatia madai ya mauaji ya watu wengi katika kanisa lake.

Katika kijiji cha kwao, Ezekiel anaelezewa kuwa mtu mkarimu na mwenye moyo mwema, ambaye katika mwaka uliopita alifadhili watoto wote wanaokwenda shule katika kisiwa hicho kidogo, ambacho kulingana na Utafiti wa Demografia na Afya nchini Kenya (KDHS), kina wastani wa watu 449

Mtandao wa Citizen Digital umeeleza kuwa Huko Ngodhe, Ezekiel alikuwa amejikita sana katika imani ya Kikristo na amewahi kuwa muumini shupavu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato la Ngodhe ambako alishiriki kikamilifu katika chama cha watafuta njia wakati wa  ujana na baadaye  kiongozi wa kwaya.

Wakaazi wa eneo hilo wanaeleza kuwa  Ezekieli alikuwa amezungumza kila mara kuhusu mipango ya kuanzisha kanisa shirikishi ambalo halingebagua dhehebu lolote chini ya dini ya Kikristo.

Alisoma katika shule ya sekondari ya Miwani huko Kisumu kabla ya kuendelea na Masomo ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Mombasa.

Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa karo ya shule, Ezekiel aliahirisha masomo yake na haikufahamika alikokuwa na kisha akaanzisha kanisa la  New Life Prayer Centre yenye makao yake Mavueni, Malindi.Hata hivyo haijulikani ikiwa alipitia mafunzo yoyote ya theolojia.

Mchungaji Ezekiel anafahamika sana na wakazi wa Ngodhe, tukio lililompatia umaarufu ni lile la  kurejea kwake katika kisiwa hicho  Oktoba 10 2022, ambapo alitua kisiwani hapo akiwa na helkopta  na kujichanganya na jamii.

Waliitaka serikali kuharakisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo wa Kituo cha New Life Prayer.Wazazi wa mhubiri huyo wamesafiri hadi Malindi.

Ezekiel Odero alikamatwa Aprili 27 mwaka huu na kufikishwa mahakamani  April 28, 2023 chini ya maombi tofauti ya kutaka kumweka kizuizini kwa siku 30.

Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kuwa watu waliokuwa wanakufa kwa kanisa lake Ezekiel walikuwa wanapelekwa kuzikwa Shakahola kwa Kanisa la Mch Mackenzie.

Citizen Digital imeeleza kuwa Mch Ezekiel Anachunguzwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ya ulaghai, utakatishaji fedha, mauaji na ukatili wa watoto.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.