MTANGAZAJI

MCHUNGAJI ALIYETARAJIWA KUKUFUKA HATIMAYE AZIKWA

 


Waumini wa Kanisa moja mjini Johannesburg, Afrika Kusini, wameripotiwa kupigwa na mshtuko baada ya Mchungaji  wao aliyefariki kushindwa kufufuka baada ya kutunzwa karibu miaka miwili katika chumba cha kuhifadhia maiti cha eneo hilo.
Kwa mujibu na ripoti ya tovuti ya habari ya  Opera, Mchungaji huyo alikaguliwa na kuthibitishwa alikuwa bado amekufa. Marafiki na familia inasemekana walitembelea mwili wa Siva Moodley katika nyumba ya mazishi ili kusali arejeshwe kwenye uhai.Lakini hilo halikufanyika, na uongozi wa nyumba ya kutunza maiti na mazishi ulilazimika kupata amri ya mahakama ili Moodley azikwe. 
Moodley, mwanzilishi wa Kituo cha Huduma ya Miujiza (MCM)huko Johannesburg, anaaminika kufariki Agosti 14, 2021, akiwa na umri wa miaka 53.
Lakini mwili wake ulisalia kuhifadhiwa katika nyumba ya mazishi ya eneo hilo kwa sababu familia yake iliamini kuwa angefufuka, kwa mujibu wa Citizen Digital.
Enzi za uhai wake , Moodley alihubiri kuhusu uwezekano wa miujiza. Kwa mujibu wa tovuti ya MCM inayodai kuwa Katika Kituo cha Miujiza, miujiza ni ya kawaida! Saratani zilizoponywa, macho ya vipofu na masikio ya viziwi kufunguliwa, miguu iliyokua na vumbi la dhahabu ni baadhi tu ya miujiza ya kawaida.
Kwa mujibu wa  meneja wa nyumba ya kutunza maiti na mazishi, Martin du Toit,familia ya Moodley ilishindwa kuudai mwili huo kwa siku 579 baada ya Mchungaji huyo  kufariki.
Martin anaeleza kuwa Wafanyakazi walifanya majaribio 28 ikiwa ni pamoja na barua pepe,Ujumbe wa WhatsApp zaidi ya mara 40, na barua za wakili kuwasiliana na mke wa Mchungaji na watoto wake ili kupata maelekezo ya nini cha kufanya na mwili wake lakini hakukuwa na majibu.
Moodley alipofariki, inadaiwa mkewe alimwambia mzikaji kwamba alikuwa na maono ambayo mumewe anaweza kufufuka,Familia iliuchukua mwili wa Mchungaji hadi kwenye nyumba ya mazishi lakini haikukubali kuzikwa au kuchomwa.
Baada ya familia kuwa kimya kwa zaidi ya mwaka mmoja, nyumba ya mazishi iliibua wasiwasi wa kuharibika kwa mazingira na kupeleka suala hilo mahakamani.Walitarajia kupata amri ya mahakama ya kumzika Moodley mwisho wa mwaka, lakini hawakuipata.
Hatimaye, mwaka huu maafisa waliamuru kwamba Moodley azikwe.Mwili wa Mchungaji huyo ulizikwa jumalililopita katika makaburi ya Westpark.Ndugu zake walihudhuria ingawa Mke wake na watoto wawili hawakushiriki mazishi hayo imeripoti News 24.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.