MTANGAZAJI

WAPROTESTANTI MAREKANI WANAONGOZA KUMUOMBA MUNGU-UTAFITI

 

Waumini wengi wa Kiprotestanti nchini Marekani hutumia muda wao wakiwa peke yao na Mungu ambapo wengi wao huzungumza na Mungu kupitia sala badala ya kumsikiliza kupitia Neno Lake, utafiti mpya umegundua.

Kwa mujibu wa  utafiti wa Taasisi ya Lifeway, 65% ya waumini wa Kanisa la Kiprotestanti  wanaokwenda kanisani hutumia muda wa peke yao na Mungu angalau kila siku, huku 44% wakisema kila siku na 21% wakisema zaidi ya mara moja kwa siku.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa 17% ya waekwenda kanisani wanasema wako peke yao na Mungu mara kadhaa kwa juma, na 7% wanasema mara moja kwa juma. Wengine walisema walitumia muda wa peke yao na Mungu mara chache kwa mwezi (5%), mara moja kwa mwezi (2%, chini ya mara moja kwa mwezi (3%) au kamwe kwa  1%

Utafiti wa Lifeway ulifanya uchunguzi mtandaoni kwa Wamarekani 1,002  kati ya Septemba  19-29, 2022,kwa kutumia jopo la kitaifa la maombi ya mwanzo ya ajira. Waliojibu walikaguliwa ili kujumuisha wale waliotambuliwa kuwa Waprotestanti ama wasio wa madhehebu na waliohudhuria ibada za dini angalau mara moja kwa mwezi.

Waumini wengi wanaohudhuria kanisani nchini Marekani, 83%, wanasema wana uwezekano mkubwa wa kuzungumza na Mungu kupitia maombi badala ya kusoma kutoka katika Biblia au Ibada (39%). Waenda kanisani wengi huomba kwa maneno yao wenyewe (83%), kumshukuru Mungu (80%), kumsifu Mungu (62%) au kuungama dhambi (49%).

Kinachoelezwa kuvutia kwa mujibu wa utafiti huo kati ya Wamarekani wanaokwenda kanisani ambao walichagua kusoma wakati wao wakiwa peke yao na Mungu, wengi walisema wangependelea kusoma kutoka katika Biblia halisi (63%). Wengine wangesoma kutoka katika Biblia inayojumuisha maelezo ya ziada  ya ibada (25%) au Maandiko kutoka kwa programu tumishi (20%). Na 7% pekee walisema watasoma ibada kutoka kwa programu tumishi.

Kwa asilimia 40, vijana wanaoenda kanisani, wenye umri wa miaka 18-34, ndio wana uwezekano mkubwa wa kusoma Maandiko kutoka kwa programu tumishi  na wana uwezekano mdogo wa kusoma kutoka katika kitabu cha ibada ambacho huchapisha Maandiko fulani (21%).

Utafiti huo unaonesha kuwa Wanawake (48%) wana uwezekano mkubwa kuliko wanaume (38%)wa  kutumia muda wao  pamoja na Mungu kuwa mazoea ya kila siku, na walioko Kusini mwa Marekani ni (49%) pia ni miongoni mwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kusema kuwa wanatumia wakati peke yao na Mungu kila siku. msingi.







No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.