TAHADHARI YA DHORUBA JIMBO LA TEXAS
Dhoruba nyingine ya msimu wa baridi inatarajia kufunika eneo kubwa la Kaskazini na Kati ya Texas katika mvua ya baridi na halijoto ya baridi, na kusababisha hali hatari za kusafiri katika sehemu kubwa ya jimbo.
Ofisi za Huduma ya Kitaifa ya Hali (NWS) ya Hewa za Dallas-Fort Worth,Austin na San Antonio zimetoa tahadhari kuhusu dhoruba ya msimu wa baridi inayohusisha kaunti nyingi kutoka Dallas kaskazini hadi Bexar kusini ambapo imefanya hivyo kwa Houston na Galveston kuhusu kuweko kwa dhoruba ya majira ya baridi katika kaunti nyingi kaskazini mwa Houston.
Tahadhari hiyo ilianza kutumika saa 3 asubuhi Jumatatu na itaendelea hadi saa 12 asubuhi Jumatano. "Vipindi kadhaa vya mvua inayoganda na baridi kali kwa siku ya Jumatatu " vilitarajiwa kutokea kwenye kaunti zilizoathiriwa katika kipindi cha siku mbili imeeleza NWS.
Kaunti za Burleson, Brazos na Washington kaskazini mwa Houston zilitarajiwa kuona vipindi vya mvua nyepesi inayoganda, na kusababisha mwangaza mwepesi, kwa mujibu wa Ofisi ya NWS ya Houston na Galveston.
Utabiri wa dhoruba ya majira ya baridi ya juma hili unafuatia dhoruba kali ya juma lililopita, ambayo ilisababisha uharibifu mkubwa wa miundo kwa nyumba na maeneo ya biashara,huku ikisababisha kukosekana kwa umeme kwa makumi ya maelfu ya wakaazi na kufungwa kwa baadhi ya barabara kuu katika eneo hilo.
Post a Comment