IDADI YA WAKRISTO UINGEREZA NA WALES YAPUNGUA
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Uingereza na Wales yaliyoachapishwa Novemba 29 mwaka huu , yanaonesha kupungua kwa idadi ya watu wanaojitambulisha kuwa Wakristo.
Mwaka 2011, watu milioni 33.2 walitambuliwa kuwa ni Wakristo. Leo hii idadi hiyo ni milioni 27.5 ambayo ni asilimia 46.2.
Akijibu matokeo hayo, Askofu Mkuu wa York, Stephen Cottrell, anasema idadi hiyo ilileta changamoto kwa Kanisa.
Anasema haishangazi kwamba Sensa inaonyesha watu wachache katika nchi hiyo wakijitambulisha kuwa Wakristo kuliko ilivyokuwa zamani, lakini bado inatupa changamoto si tu kutekeleza wajibu wetu. katika kumfanya Kristo ajulikane.
Licha ya kuporomoka kwa utambulisho wa Kikristo, Askofu Mkuu huyo anasema kuwa Kanisa litaendelea kuwepo kwa ajili ya Taifa wakati wa shida.
Asilimia ya watu wanaosema hawakuwa na dini imeongezeka katika muongo mmoja uliopita kutoka karibu robo ya watu (asilimia 25.2) hadi zaidi ya theluthi moja mwaka wa 2021 (asilimia 37.2).
Idadi ya watu wanaojitambulisha kuwa Waislamu ilipanda kutoka asilimia 4.9 hadi asilimia 6.5 mwaka jana.
Mkuu wa Utafiti wa Chama cha Biblia Dkt Rhiannon McAleer, anasema data inaonyesha kwamba utambulisho wa kidini nchini Uingereza na Wales bado ni "mkuu" na "uko juu".
Utafiti zaidi wa Chama cha Biblia unaochunguza imani ya kidini kati ya 2018 na 2022 haukupata kuwa kupungua kwa imani ya Kikristo kumesababisha ongezeko la kutokumtambua Mungu.
Sensa hiyo pia iligundua kupungua kwa idadi ya watu nchini Uingereza na Wales wanaojitambulisha kuwa wazungu, kutoka asilimia 86 miaka 10 iliyopita, hadi asilimia 81.7 mwaka jana.
Post a Comment