MTANGAZAJI

WAADVENTISTA AUSTRALIA NA MPANGO KWA VIJANA

 


Unioni Konferensi ya Austrialia ya Kanisa la Waadventista wa Sabato   (AUC)  Imezindua mpango wa  Uongozi na Utume uliojikita katika maisha,mradi ambao unalenga kufikia wanafunzi wa vyuo vikuu visivyo vya  kanisa na kutoa msaada kwa wanafunzi wa Kiadventista  wanaosoma katika vyuo vikuu visivyomilikiwa na Kanisa hilo.
Mpango huo wa miaka minne utawaweka vijana wawili katika vyuo vikuu vilivyochaguliwa ambavyo siyo vya Kiadventista nchini  Australia katika juhudi za kuanzisha vikundi vya maisha kwenye chuo kikuu.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa Kundi la Barna, asilimia 72 ya vijana wanaohudhuria kanisani huko Australia huacha maisha ya kanisa wanapoingia chuo kikuu na katika umri wa ujana.
Lengo la mpango huu ni kuwasaidia vijana wa Kiadventista kubaki kanisani na kuwezesha kuwafikia wanafunzi wa vyuo vikuu visivyo vya kiadventista nchini humo.
Viongozi wa Kikundi cha Maisha watakuwa na ufadhili wa rasilimali zinazohitajika kuwezesha vikundi vya maisha vipya, ikiwemo  mafunzo na usaidizi kutoka kwa washauri katika kila ngazi, kutoka kanisa la mtaa hadi Divisheni ya Pasifiki ya Kusini ya Kanisa la Waadventista.
Jeffrey Parker, mkurugenzi wa vijana wa AUC, anasema, "Inafurahisha sana kuona mikutano yao yote ya Australia inataka kuwa sehemu ya pendekezo hili la huduma ya Kikundi cha Maisha linapoanza 2023/24.
AUC inashughulikia kutengeneza tovuti mpya ambayo itakuwa mtandaoni katikati ya Desemba mwaka huu.Tovuti hii itawapa wazazi, walezi,babu,bibi, marafiki, na wanafunzi wa Vyuo Vikuu  fursa ya kufahamisha mahali wanaposoma na kuwasaidia kuunganishwa na vijana wengine wazima wa Kiadventista katika eneo hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.