MTANGAZAJI

YOHANA 3:16 YAONGOZA KWA KUTAFUTWA ZAIDI


 

Yohana 3:16 ndio mstari maarufu zaidi wa Biblia duniani kwa sasa, kwa mujibu wa uchunguzi wa kidijitali wa World Vision.

Mstari huo unasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Utafiti wa kimataifa ulikagua data kutoka kwa zana ya kutafuta neno kupitia  ahrefs.com ili kupata wastani wa kila mwezi wa kutafuta kwa njia ya Google kwa nchi 172.

Pia ilizingatia data ya utafutaji wa Google wa nchi moja na nyingine kwa mistari 100 ya Biblia inayosomwa zaidi kwenye tovuti maarufu ya usomaji wa Biblia kwa mujibu wa tovuti ya Bible Gateway.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Yohana 3:16, ilikuwa na utafutwaji wa kila mwezi zaidi wa watu milioni 2.1 ulimwenguni pote, ikifuatwa na Yeremia 29:11 na Wafilipi 4:13 kwa sekunde 82,000. Huku Yohana 10:10 ikiwa nafasi ya tatu kwa kutafutwa mara  73,000 wa kila mwezi.

Ikigawanywa kutokana na nchi, Yohana 3:16 ulikuwa mstari wa Biblia chaguo bora kwa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Australia, Canada, Nigeria, Afghanistan, India, Ufilipino, Somalia na Ethiopia.

Katika  nchi za Amerika ya Kusini, watu wameonesha idadi kubwa ya  kutafuta Mwanzo 1:27, "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu aliwaumba, mwanamume na mwanamke.

Nchini  Uingereza fungu la Yohana 3:16 limetafutwa mara  6,500 wa kila mwezi, ikifuatiwa na Yeremia 29:11 (mara 2,000  kila mwezi) na Yohana 14:6 (mara  1,900 wa kila mwezi).

Utafiti huo pia uligundua kuwa Yohana 3:16 imesambazwa sana katika mitandao ya kijamii. Hushtag ya  #John316 iliyoangaziwa katika machapisho zaidi ya 250,000 ya Instagram na imetazamwa zaidi ya mara milioni 55.9 kwenye TikTok.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.