MTANGAZAJI

KIONGOZI WA WAADVENTISTA ATAKA VIJANA KUPEWA NAFASI ZA UONGOZI

 


Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventist wa Sabato katika Divisheni ya Amerika Kaskazini  (NAD)  Glenward Alexander Bryant amesema ni muhimu matumizi ya vyombo vya habari vya kidigitali  yaongezeke  katika kutangaza utume wa kanisa hilo.

Amesema angependa kuongeza wamishenari 10,000 wa kidijitali kushawishi mitandao ya kijamii na kupanua ushirikiano wa vyombo vya habari katika Divisheni hiyo ,kwa kuwa  itakuwa njia ya ubunifu kwa vijana kufanya uinjilisti na kuliongoza kanisa.

Ili kukua kwa kasi,Wenyeviti wote wa Konferensi wamekubali kuongoza fursa ya uinjilisti wa hadhara ndani ya maeneo yao na kuwahimiza walei kushiriki katika juhudi zaidi za kuwafikia watu.

Ameeleza kuwa Viongozi wa kanisa wanapostaafu, ni muhimu vijana wakuzwe kwa makusudi katika nyadhifa za uongozi.

Moja ya mambo makuu ya ripoti ya Bryant aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa NAD uliomalizika hivi karibuni ilikuwa ni kuwa na "vituo vya mvuto" ambako Miji ishirini nchini Marekani ina 50% ya idadi ya watu walioko katika Divisheni hiyo,Ni lengo la NAD ni kupanua uwepo wa Waadventista katika miji hii. Amerika Kaskazini huongeza idadi ya watu kwa milioni 1.5 kwa mwaka,hata hivyo, kanisa la Waadventista hukua kwa 35,000 tu kwa mwaka (kwa wastani). Divisheni ingependa kuona idadi hii ikiongezeka hadi 50,000.

Takwimu za Divisheni hiyo  zinaonesha kuwa kati ya Waadventista 1,271,642 katika NAD (mwishoni mwaka 2021), 68% kati yao wako chini ya umri wa miaka 60.Walakini, 32% ya wenyeviti  wa NAD wameshazidi umri wa kustaafu, na zaidi ya 50% wana  umri wa zaidi ya miaka 60.

Kwa mujibu wa  utafiti wa kustaafu wa Waadventista miaka tisa iliyopita, kati ya wachungaji 4,000 walioajiriwa na kanisa hilo, asilimia 50 watakuwa wamestaafu kufikia mwaka ujao.
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.