MTANGAZAJI

SHIRIKA LA WAADVENTISTA LATOA MSAADA KWA WAHAMIAJI

 

 Shirika la Waadventista la maendeleo na utoaji wa misaada wakati wa majanga (ADRA), kwa uratibu na wataalamu wa afya wa Waadventista na watu wa kujitolea kutoka Chuo Kikuu cha Autonomous cha Baja California, Mexico, wamefanya huduma za matibabu kwa makumi ya wahamiaji huko Tijuana.
Mpango huo wa ADRA, ulioanza Machi 2022, unalenga kuwasaidia wahamiaji kwa huduma za matibabu zinazohitajika sana.
Wahamiaji hawa wameziacha nchi zao za Haiti, Honduras, Nicaragua, Guatemala, El Salvador, na majimbo mengine nchini Mexico, na sasa wanatafuta makazi ya muda wanapojaribu kuhamia kaskazini mwa Marekani.
Wafanyakazi wa kujitolea 50 walitoa huduma ya lishe, huduma za meno, na usaidizi wa kisaikolojia na kijamii, pamoja na shughuli mbalimbali  kwa watoto ambapo Wafanyakazi wa kujitolea waliratibiwa na kikundi kutoka kwa Kitengo cha Dharura cha ADRA kwa ushirikiano na Idara ya huduma za Afya ya Waadventista katika eneo hilo.
Carlos King Mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura Wataalamu wachache wa afya husafiri mara moja au mbili kwa mwezi au wakati mwingine zaidi kutoa huduma kwa dazeni au zaidi ya wahamiaji katika saa nne wanazotembelea makao hayo.
Tijuana ni moja ya eneo kuu linalotumiwa na wahamiaji kuvuka mpaka huko Mexico,kwa mujibu wa mamlaka ya serikali ya Baja California, mnamo mwaka 2021 zaidi ya wahamiaji 31,000 walitambuliwa katika ofisi za uhamiaji au makazi. Idadi ya wanaopita kuelekea kaskazini ina uwezekano mkubwa kuliko ilivyoripotiwa rasmi.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.