MTANGAZAJI

MAKANISA YAOMBWA KUPINGA UTUMWA

 


Wakati mijadala ya ukosoaji wa mashindano ya Kombe la Soka la Dunia ikiendelea kutokana na uwepo wa ripoti za usafirishaji haramu wa binadamu, kazi za kulazimishwa na mazingira ya kazi yasiyo ya haki yakiwaathiri wafanyakazi nchini Qatar, mwenyeji wa michuano ya mwaka kuu.
Taasis ya Haki ya Kimataifa IJM na  Taasis ya utoaji misaada kwa wanaonyanyaswa zote za nchini Uingereza zimezindua mpango wa utetezi ambao unaohimiza makanisa kusaidia kulinda watu walio katika hatari ya kunyonywa kote ulimwenguni kupitia kuandaa matukio ya uhamasishaji wa uelewa na uchangishaji wa fedha wakati michuano hiyo mikubwa ya mchezo wa soka unaelezwa kuwa na mashabiki wapatao bilioni 5 duniani.
Taasisi hizo zinataka kuongeza ufahamu wa ukweli kwamba kazi za kulazimishwa na aina nyingine za unyonyaji hutokea kila mahali - sio tu nchini Qatar pekee na kuchukua hatua chanya kukomesha.
Taarifa ya taasisi hizo inaeleza kuwa huu ni mwaka  2022, ulimwengu uko katika wakati mbaya katika safari ya kutokomeza utumwa, huku hali ikizidi kuwa mbaya.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Shirika la Kazi Duniani,ILO  watu milioni 28 kote ulimwenguni sasa wamenaswa katika kazi za kulazimishwa, ongezeko la milioni 2.7 tangu 2016 - ongezeko ambalo ILO inahusisha na athari za pamoja za janga la Covid-19, migogoro na mabadiliko ya hali ya hewa.
Taarifa ya taasisi hizo inaeleza kuwa Kazi ya kulazimishwa ni aina ya utumwa wa kisasa unaojumuisha kazi ya kulazimishwa katika ujenzi, hoteli na tasnia zingine zinazohusiana na hafla za michezo.Kichocheo kimoja kikuu cha utumwa ni umaskini, kwani unawafanya watu kuwa katika hatari ya kupata ofa za uwongo za kazi, ambazo wafanyabiashara huzitumia kuwanasa katika mazingira ya unyonyaji.
Ingawa Kombe la Dunia limeweka kipaumbele juu ya unyonyaji nchini Qatar, ukweli ni kwamba kazi ya kulazimishwa na aina nyingine za utumwa hutokea kila mahali.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.