MTANGAZAJI

MHAZINI WA KANISA AFUNGWA KWA WIZI FEDHA ZA KANISA

 


Mweka Hazina wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Pretoria nchini Afrika Kusini amefungwa  jela miaka mitatu baada ya kuiba R800,000 kutoka kwa hazina ya kanisa hilo.

Mahakama maalumu ya masuala ya Biashara ya mjini Pretoria nchini Afrika Kusini hivi karibuni  ilimhukumu Lady Memory Mutsika, 43, kifungo cha hicho baada ya kumpata na hatia ya makosa 128 ya wizi.

Mutsika raia kutoka Zimbabwe  alikuwa mweka hazina wa kanisa hilo na majukumu yake ni pamoja na kuhamisha zaka na sadaka  zilizowekwa kwenye akaunti ya kanisa, kwenda kwa hazina ya Konferensi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato. 

Msemaji wa Mamlaka ya Kuendesha Mashtaka Lumka Mahanjana ameeleza kuwa Katika kipindi cha miaka minne kuanzia 2012 hadi 2015, Mutsika alihamisha zaidi ya R800,000 kati ya pesa alizopokea kutoka zaka na sadaka kwenda kwenye akaunti yake ya benki na kwa matumizi yake binafsi.

Mahakamani, Mutsika alikiri mashtaka hayo na kuomba apewe kifungo cha kutozuiliwa ili kulipa kanisa hilo pesa hizo kwa muda wa miaka mitano.

Mahanjana amesema Hata hivyo, serikali ilisema kuwa Mutsika kila mara alionyesha nia yake ya kulipa pesa hizo na hajalipa hata senti moja tangu Machi 2022, baada ya kukutwa na hatia. Hakimu alikubaliana na serikali na kusema Mutsika hakuonyesha majuto.




 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.