MTANGAZAJI

UTAFITI-HALI NGUMU YA MAISHA UINGEREZA

 

Uingereza inakabiliwa na mzozo wa deni la dharura huku wengi wakigeukia kukopa ili kupata pesa katika miezi ya msimu wa baridi, shirika la kutoa misaada la Kikristo limesema.
Utafiti wa Taasisi ya Kikristo inayopambana na umaskini (CAP) unaonyesha kuwa kote Uingereza, watu wengi ambao ni 84% wameathiriwa kifedha na gharama ya shida ya maisha.
Kwa karibu nusu ya wale waliohojiwa na CAP asilimia 49, bili zao na gharama zimeongezeka kwa kati ya £ 101 na £ 500 kwa mwezi.
Chini ya nusu tu yaani asilimia 48 wanasema wanatatizika kifedha na watatu kati ya watano ambayo ni asilimia 61 wamepunguza matumizi ya nishati katika jitihada za kuokoa pesa.
Zaidi ya mmoja kati ya 10 ikiwa ni asilimia 13 wako nyuma kwenye bili za kaya na wawili kati ya watano ambayo ni asilimia 42 wamekopa fedha ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha.
Baadhi ya 16% wanaacha  mlo mmoja na idadi sawa (15%) inakadiriwa kuwa haipati joto au umeme kabisa. Zaidi ya theluthi moja (37%) wamekatisha shughuli za kijamii na starehe kabisa.
Mmoja kati ya 10 (13%) ya waliokopa alisema hawajui itawachukua muda gani kurejesha mikopo.
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CAP, Gareth McNab, anasema kuwa matarajio ya kuongezeka kwa gharama za nishati msimu huu wa baridi ni "ya kutisha".
Utafiti huo uliidhinishwa na CAP na kufanywa na YouGov na sampuli ya uwakilishi wa kitaifa ya watu 2,270 mnamo Agosti 2022.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.