MTANGAZAJI

BIASHARA KATI YA TANZANIA NA NIGERIA YAONGEZEKA


 

Biashara kati ya Tanzania na Nigeria imeongezeka kutoka shilingi bilioni 23 mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 24 mwaka 2021. 

Takwimu hizo zimetolewa hivi karibuni katika hafla ya  maadhimisho ya maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Nigeria yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam Tanzania.

 Takwimu za biashara na uwekezaji zinaonesha kuwa  kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbli mbili kimeendelea kuongezeka, kutoka shilingi bilioni 23 mwaka 2020 hadi shilingi bilioni 24 mwaka 2021. Kuhusu uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili Kampuni 23 za Nigeria ambazo zimewekeza Tanzania kwa uwekezaji wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 466.50 na kutoa takriban ajira 1,734.

Tanzania na Nigeria zinashirikiana kwa karibu kukuza Ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Afrika. Hii inalazimu, miongoni mwa mambo mengine, kukuzwa kwa jamii zenye amani, usawa, na ajenda ya maendeleo ya bara la Afrika na watu wake.

 Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Hamisu Umar Takalmawa amesema kuwa Nigeria inajivunia kuwa rafiki wa Tanzania kwani mataifa haya yamekuwa yakishirikiana kijamii katika masuala ya utamaduni, muziki, nyimbo na tamthilia

“Ushirikiano na umoja baina ya Nigeria na Tanzania umekuwa na misingi imara ya kukuza na kuimarisha diplomasia baina ya mataifa yetu mawili,” amesema Balozi Takalmawa

Balozi Takalmawa ameongeza kuwa biashara kati ya Nigeria na Tanzania imeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita, kadhalika uwekezaji nao umeongezaka jambo ambalo linaashiria mazingira bora ya biashara na uwekezaji.




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.