MTANGAZAJI

MWIMBAJI NA MWANZILISHI WA KITUO CHA TELEVISHENI CHA BREATH OF LIFE AFARIKI DUNIA

 

 

Mwanzilishi wa Kituo cha Televisheni cha Breath of Life cha nchini Marekani ambacho hutoa vipindi vya maudhui ya Ki Adventista ,Walter E. Arties amefariki dunia,kifo cha Walter aliyezaliwa Novemba 1941 na mmoja wa waanzilishi wa Kikundi cha uimbaji cha Breath of Life Quartet kimetangazwa mchana wa Juni 26,2022 kupitia mitandao ya kijamii ya Breath of Life TV na Kanisa la Wa Adventista wa Sabato la Chuo Kikuu cha Oakwood.

Kwa siku kadhaa kupitia gazeti la mtandaoni la Kituo cha Televisheni cha Breath of Life kimekuwa kikitoa taarifa ya  kuungana katika maombi maalum ya kumuombea Walter Arties aliyekuwa mgonjwa.

Wakati wa uhai wake Walter ambaye pia alikuwa mwimbaji wa solo,amewahi kuonekana kwenye video kadhaa za waimbaji wa VOP Family Reunion.akiwa na waimbaji wenzake mwaka 1974 alianzisha kikundi cha Breath of Life Quartet kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji kwenye kituo cha Televisheni cha Breath of Life.

Mwaka 2001 Walter Arties alikuwa nchini Tanzania ambapo yeye pamoja na waimbaji wengine kutoka Marekani na nchi mbalimbali za Afrika walishiriki kutoa huduma ya uimbaji kwa Mkutano wa Injili uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza uliokuwa na jina la Africa for Christ 2001 uliorushwa kwa njia ya satalaiti na Adventist World Television (AWT) kwa sasa Hope Channel International na Adventist Global Communication Network (AGCN)



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.