MTANGAZAJI

AUDREY ANDERSSON AWEKA REKODI YA UONGOZI KWA WA ADVENTISTA

 


Pamoja na kuchaguliwa kwa Audrey Andersson kwa nafasi ya  Makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni  wa Konferensi Kuu (GC), hakuna wanawake katika nafasi tatu za juu za uongozi wa Kanisa hilo (Mwenyekiti, Katibu, na Mweka hazina) hata katika Divisheni  13  za Kanisa hilo Duniani.
Divisheni ni ngazi ya pili ya juu ya kiutawala katika Kanisa la Wa Adventista Ulimwenguni ambapo  GC pekee ndio iko juu.Makao Makuu ya GC yako nchini Marekani.
Kabla ya kuwa makamu wa GC, Andersson alikuwa Katibu Mtendaji wa Divisheni ya Trans-European (TED) tangu mwaka 2010,mwanamke pekee ambaye amewahi kushika  nafasi hiyo kwa ngazi ya Divisheni katika kanisa hilo. TED ina jumla ya waumini  88,533 wa kanisa hilo, ambapo kati yao asilimia 61 ni wanawake na asilimia 39 ni wanaume.
Kwa sasa, Andersson ndiye makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato wa GC mwanamke pekee kati ya makamu saba waliochaguliwa mwaka huu. Ella Simmons, Makamu mkuu wa kwanza mwanamke wa GC, aliyestaafu mwaka huu baada ya kutumikia nafasi hiyo tangu mwaka 2005.
Nafasi za juu za Uongozi wa Kanisa la Wa Adventista wa Sabato Ulimwenguni zote zinaongozwa na wanaume, Hata hivyo, kwa mujibu wa toleo la tatu la takwimu za mwaka 2021 za Kanisa lenyewe, zinaonesha kuwa wanawake ni wengi zaidi kuliko wanaume katika Kanisa la Waadventista wa Sabato ambapo wanawake ni asilimia 57 na wanaume ni asilimia 43
Hadi Disemba 31,2021 kwa mujibu wa  tovuti ya Kanisa la Wa Adventista wa Sabato,kulikuwa na waumini  21,912,161 wa kanisa hilo Duniani,kukiwa na makanisa 95,297.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.