MTANGAZAJI

SERIKALI YAFUNGULIA MAGAZETI YALIYOFUNGIWA

 

 Serikali ya Tanzania  imeyafungulia magazeti manne baada ya kufungiwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.
 
 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania Nape Nnauye amewaambia   wahariri wa vyombo vya habari na waandishi wa habari kuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuagiza kuyafungulia magazeti yaliyofungiwa na agizo hilo n linakuwa ni sheria, na sheria inatekelezwa.

“Leo natoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa ambayo ni Mseto, Mawio, Tanzania Daima na Mwanahalisi, hivyo ni vizuri kuondoka kwenye maneno tutende, na leseni hizo nazikabidhi leo, kifungo kimetosha, Kazi iendelee,” amesisitiza Waziri Nape.

"Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita  kwenye tasnia hii ni kuwa karibu nanyi, tuzungumze kwa kuwa ninyi ni wadau kwenye maendeleo ya taifa letu, semina hizi zirekodiwe, mawazo ya wanahabari yachukuliwe vizuri, ili viongozi tuyachukue na kuyafanyia kazi, tunataka tuboreshe mahusiano yaliyopo katika ya Sekta ya Habari na Serikali, ambapo ameleekeza tupitie sheria, taratibu na kanuni ili ziwe rafiki na kuwezesha utendaji kazi wa wanahabari badala ya kuwa kikwazo kwa wanahabari"Amesema Nape

Said Kubenea wa magazeti ya Mseto na Mwanahalisi ameishukuru Serikali na kwa hatua hiyo ya kufungua magazeti haya ambapo amesema magazeti hayo  yalimaliza adhabu zaidi ya miaka miwili iliyopita na yalishinda kesi ila hayakuweza kurudi mtaani huku akisisitiza kuacha yaliyopita ambapo ameahidi   kufanya kazi kwa kuangalia maslahi ya taifa la Tanzania kwa kuzingatia weledi, maadlii na utendaji wa kazi zao.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.