WATOTO 981 WAPEWA UJAUZITO WILAYANI KIBONDO
Vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto vimebainika kukita mizizi katika Wilaya ya Kibondo,Kigoma nchini Tanzania ambapo ripoti ya Wilaya hiyo inaonesha kuwa watoto 981 wamepewa ujauzito katika kipindi cha miezi sita, Januari mpaka Juni 2021.
Taarifa hiyo imebainika wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiwa wilayani humo kukagua na kujionea utoaji wa huduma za ustawi wa Jamii na masuala ya maendeleo ya jamii.
Naibu Waziri Mwanaidi amesema taarifa hizo haziwezi kufumbiwa macho na badala yake watendaji wanaohusika wafanye kila linalowezekana kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana na haki inatendeka katika kipindi kifupi iwezekanavyo.
Naibu Waziri Mwanaidi ameongeza kuwa jamii haiwezi kutegemea miujiza ya mafanikio ya kizazi kijacho endapo itabaki kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani dhidi ya wanawake na watoto kwa kuangalia watoto wao wanapata mimba katika umri mdogo na kukatisha ndoto zao.
Post a Comment