TAHADHARI YA COVID-19:OBAMA APUNGUZA IDADI YA WAALIKWA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Rais wa 44 wa Marekani Barack Obama amepunguza idadi ya wageni wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mwishoni mwa juma kutokana na tahadhari ya virusi vya Covid-19 ambapo atakuwa anatimiza miaka 60.
Msemaji wa Obama, Hanna Hankins, ameviambia vyombo vya habari kuwa Rais huyo msataafu atapunguza idadi hiyo ikiwa ni tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya kirusi cha corona.
"Kutokana na hali ya maambukizi kuongezeka toka juma lililopita familia ya Obama imeamua kulipunguza tukio hilo na hivyo kuhusisha wanafamilia na marafiki wa karibu peke yake"amesema Hankins.
"Anashukuru kwa wote wanaomtumia ujumbe wa kheri ya siku yake ya kuzaliwa kutoka mbali na anataraji kuwaona hivi karibuni ."
Awali ilielezwa kuwa, Obama aliyezaliwa Agosti 4, 1961 angeongoza sherehe hizo siku ya jumatano katika visiwa vidogo vya Martha's Vineyard Massachusetts
Imeelezwa kuwa mamia ya wageni waliokuwa wamealikwa walipaswa kuonesha uthibitisho wa kipimo cha kuonesha kuwa hawana virusi vya Covid-19 kwa ajili ya kuhudhuria tukio hilo na kufuata miongozo ya kujikinga na Corona kwa kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka.
Watu maarufu akiwemo Oprah Winfrey na George Clooney, walikuwa wametajwa kuhudhuria .
Afisa wa Ikulu ya Marekani alisema jumanne kuwa Rais wa Marekani Joe Biden hatohudhuria sherehe hiyo,japo anataraji atakutana na Obama hivi karibu na anamkaribisha katika jumuia ya watu wenye miaka 60.
Post a Comment