MTANGAZAJI

CHANJO YA ZIADA YA COVID-19 MAREKANI


Maafisa wa Sekta  ya Afya wa Marekani jumatano hii wametangaza mpango wa kusambaza chanjo ya dozi ya ziada ya  Covid-19 kwa wamarekani ikiwa ni njia ya kujikinga na kirusi aina ya Delta kinachosababisha Corona.   
 
Mpango huo ambao umefafanuliwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa (CDC) Dkt. Rochelle Walensky kwa kushirikiana na Mamlaka zingine za Afya,wamehimiza utoaji wa dozi ya ziada miezi nane baada ya mtu kupatiwa chanjo ya pili ya Pfizer au  Moderna ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza kufanyika Septemba 20 mwaka huu.
 
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa mtu aliyechanjwa  dozi moja ya  chanjo ya Johnson & Johnson huenda naye akahitaji dozi ya ziada ingawa maafisa wa Afya wanasema wanasubiri data zaidi na watahitaji kupata maelezo zaidi.
 
"Mpango wetu ni kuwalinda wamarekani na kuwakinga dhidi ya kurusi"amesema Mkurugenzi wa CDC Dkt . Rochelle Walensky .
 
Mpango huo sasa unasubiri tathimini ya usalama na ubora wa chanjo ya ziada toka kwa Uongozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa,imeeleza taarifa hiyo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.