MTANGAZAJI

WABUNGE TANZANIA WASHAURI SOMO LA SAYANSI KIMU KUREJESHWA SHULENI

 

Wabunge nchini Tanzania  wameishauri Serikali kurudisha shuleni somo la Sayansi Kimu ili watoto wafundishwe kuandaa lishe bora tangu wakiwa watoto, jambo ambalo litasaidia kupambana na athari zitokanazo na lishe duni.

Akizungumza katika semina lishe kwa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG), iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani, Mbunge wa Urambo  Magareth Sitta alisema zamani watoto walifundishwa juu ya kutayarisha chakula lakini hivi sasa hawajifunzi tena.

“Serikali kwanini wameondoa somo la domestic sience (sayansi kimu) sisi wengine tulijifunza kule namna ya kuandaa chakula. Na kwanini wanafunzi hawana mashamba ya shule,”alisema.

Mbunge wa Viti Maalum Anna Lupembe aliunga mkono kauli ya Sitta ambaye alitaka wataalam wa lishe kutembea katika halmashauri kwa ajili ya kutoa elimu ya lishe bora.

Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo alisema suala la lishe ni muhimu sana halifai kuchukuliwa kiwepesi.

Alitaka suala la lishe na magonjwa ya kuambukizwa kupelekwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu ili yaweze kuratibiwa kikamilifu.

Mkurugenzi wa shirika hilo Neema Lugangira alisema udumavu unaotokana na lishe duni unasababisha uwezo mdogo wa kufyonza virutubishi  na uyeyushaji wa chakula.

Alitaja athari nyingine ni riski ya kupata magonjwa mbalimbali hasa ya kuambukiza, kuugua mara kwa mara kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia, gharama kubwa ya matibabu.

“Ongezeko kwa kasi ya ugonjwa mfano Ukimwi kiwemo mama mwenye Ukimwi kumuambukiza mtoto Ukimwi. Elimu duni haswa kwa vijana,”alisema.

Alisema udumavu unaweza kupunguza uwezo wa kufikiri wa mtu na upungufu wa madini joto, unaweza kupunguza, kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu na upungufu wa wekundu wa damu

Mbunge wa Viti Maalum  Dk Thea Ntara alishauri wataalam wa lishe nchini kufanya utafiti wa vyakula vinavyoweza kumpatia mtu vitamin E.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.