WATANZANIA WATAKIWA KUNUNUA BIDHAA ZENYE ALAMA YA UBORA
Ngenya aliyasema hayo eneo la Mwahako Jijini Tanga katika maonyesho ya nane ya Biashara ambapo alisema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea hasara ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kutokana na bidhaa wanazonunua kutokuwa na ubora unaotakiwa.
Alisema bidhaa zimekuwa na athari nyingi katika matumizi ya binadamu hivyo ni muhimu watanzania kutambua kwamba wanaponunua bidhaa wanapaswa kuzikagua na kuona kama zina ubora unaotakiwa ili kuweza kuepukana na majanga ambayo yanaweza kuwakuta kutokana na bidhaa feki.
“Lakini hata katika operesheni zetu ambazo tumekuwa tukizifanya tunagundua bidhaa gani ambazo zinaingizwa kwenye masoko na hazina ubora ikiwemo bidhaa za ujenzi ,vifaa vya umeme vingi vinakuja feki hivyo tujitahidi kuvitambua na kuviondoa kwenye soko kwani mfano vifaa vya umeme madhara yake vinaweza kushika moto na kuweza kuharibu mali”Alisema Mkurugenzi huyo wa TBS
Post a Comment