MTANGAZAJI

INSTAGRAM WAJA NA MPANGO WA INSTAGRAM KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 13

Watu wenye umri chini ya miaka 13 hawawezi kujiunga na mtandao wa instagram katika baadhi ya nchi  mfano Marekani ambapo sheria haziwaruhusu kufanya hivyo,ingawa zuio hilo haliwazui kujiunga na mtandao huko kwani wapo wanaoongopa umri wao kwenye mitandao.

 Instagram wanasema wamekuja na suluhisho ambalo huenda litawahusu watoto ambao watajiunga na mtandao huo wa kijamii wakiwa na umri mdogo.Kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kutengeneza jukwaa la Instagram iitwayo Instagram Youth
 
"Kuna idadi kubwa ya watu wenye umri chini ya miaka 13 ambao wangehitaji huduma kama ya Instagram,Kwa sasa haturuhusu wao kufanya hivyo"ameeleza Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook na Instagram .Ripoti iliyotolewa na taasisi ya Thorn inaonesha kuwa asilimia 40 ya watoto chini ya miaka 13 wanatumia Instagram.
 
Suluhisho la Zuckerberg ni kutengeneza  Instagram kwa watoto 'Instagram Youth" ikiwa na mpangilio wa uangalizi wa wazazi. Japo bado haijalikana mtandao huo utakavyokuwa ukifanya kazi.Pia bado hajawekwa wazi sababu hasa ya kuwafanya watoto chini ya miaka 13 kujiunga na mtandao wa kijamii ingawa inaelezwa kuwa huenda ni katika kushindana na Snapchat ama TikTok ambazo zinatumiwa na vijana kwa sasa ingawa zinaudhibiti wa umri.
 
Hata hivyo wanasheria wakuu kutoka katika majimbo 44 nchini Marekani wameitaka Facebook kuachana na mpango huo ili kuwalinda watoto.
 
Takwimu za Mtandao wa Statista za mwaka 2021 zinaonesha kuwa Januari 2021 kulikuwa na asilimia 14.5 ya watu wote duniani wanaotumia Instagram ambao ni wanawake wenye umri kati ya miama 18 hadi 24.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.