MTANGAZAJI

MIKUTANO YA GAiN 2021 TANZANIA NA ULAYA



Mikutano inayowakutanisha Wataalamu wa Habari na Teknolojia ya Mawasiliano katika Kanisa la Waadventista Ulimwenguni ambao wamejikita kwenye matumizi ya Intaneti katika kupeleka utume wa Kanisa hilo GAiN imefanyika katika nchi mbalimbali Duniani.
 
GAiN 2021 nchini Tanzania Kanisa hilo limewakutanisha wadau hao Mjini Morogoro Tanzania  ikiwemo Wakuu wa Taasisi, Wachungaji,Wazee wa Makanisa,Makarani,Makatibu Muhtasi,Wataalamu wa Mifumo ya Teknohama,Wasimamizi wa Teknohama,Viongozi wa Kanisa katika majimbo yote ya Kanisa hilo, wafanya kazi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista TAMC  na wadau wote wa Teknohama kuanzia April 27 hadi Mei Mosi mwaka huu ambapo kauli mbiu yake ni Kuikabili Miisho ya Wakati Kidigitali.
 
 Jumatatu Aprili 19, 2021,huko Ulaya kulifanyika mkutano wa GAiN 2021.Ambako kwa mwaka huu mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao kutokana na uwepo wa janga la Corona,takribani washiriki 100 walijitokeza ikiwemo Wanataaluma,Viongozi na wafanyakazi katika sekta ya Teknohama miongoni mwao wakitokea Ulaya,Asia, Afrika, na Amerika.
 
 GAiN 2021 imeratibiwa na Divisheni mbili za Ulaya katika Kanisa la Waadventista na kusimamiwa na Wakurugenzi wawili wa Idara ya Mawasiliano Corrado Cozzi  Victor Hulbert kwa ushirikiano na Hope Media Europe inayosimamiwa na  Klaus Popa
 


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.