MTANGAZAJI

MAUZO YA BUNDUKI YAONGEZEKA MAREKANI


Mauzo ya bunduki nchini Marekani yameonesha kuongezeka  katika kipindi cha mwaka 2020 kwa mujibu wa takwimu za serikali na watengenezaji wa silaha hizo  nchini humo.

Takwimu hizo zilizotolewa Januari 5,2021 zinaonesha kuwa takribani bunduki milioni 23 zilinunuliwa kwa mwaka 2020 kwa mujibu wa Taasisi ya Uchambuzi wa takwimu za  silaha ndogo (SAA) iliyoko Greenville, South Carolina.

Idadi hiyo ni ongezeko la asilimia 65 ukilinganisha na kipindi cha mwaka 2019, ambapo bunduki milioni 13.9 ziliuzwa , kwa mujibu wa takwimu za Taasisi hiyo.

Mwezi Machi mwaka 2020 FBI ilifanya ukaguzi wa umiliki wa bunduki zaidi ya milioni 3.7 katika mwezi ambao uliingiliana na karantini iliyotokana na  janga la Corona,idadi hiyo inaelezwa ni ongezeko la bunduki milioni moja kwa ukaguzi uliofanyika Machi 2019.

Takwimu za ukaguzi wa silaha za moto kwa mwaka 2020 katika jimbo la  Georgia ulionesha wakazi  904,035, ambalo ni ongezeko la 68% tangu   mwaka 2019. Jimbo la Michigani lilionesha ongezeko la  155% tangu januari mwaka 2019 huku jimbo la New Jersey likionesha ongezeko la asilimia  240% katika kipindi cha Januari 2019 hadi Januari 2020.

 

 

 

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.