MTANGAZAJI

SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA GAWIO LA BILIONI 32.9 KUTOKA AIRTEL

 


Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania Plc, imeilipa Serikali ya Tanzania, shilingi 32.9 bilioni kama gawio na mchango maalum wa maendeleo baada ya kupata faida katika Mwaka wa Fedha 2019/20.

 

Mfano wa Hundi mbili za fedha hizo Fedha hizo ziliwasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Airtel Tanzania Plc, Bw. Gabriel Malata na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ndiye mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Doto James, Jijini Dodoma.

 

Akikadidhi hundi hiyo, Bw. Malata alisema katika kiwango hicho cha Shilingi Bilioni 32.99, Shilingi Bilioni 18.99 ni gawio na shilingi bilioni 14 ni mchango maalum wa maendeleo kwa Serikali baada ya Kampuni hiyo kupata faida ya bilioni 38.5 kwa mwaka unaoishia Disemba 2019/2020.

 

Akieleza mafanikio yaliyosababisha Kampuni yake kutoa gawio hilo na michango ya maendeleo ya shilingi Bilioni 1 kila mwezi, Bw. Gabriel Malata alisema licha ya uwekezaji mzuri katika upanuzi wa mtandao, idadi ya wateja imeongezeka kutoka milioni 11.4 Machi 2019 mpaka 13.3 milioni Machi 2020 na kwa sasa umiliki wa soko ni asilimia 27 kwa taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

 

Imeelezwa  kuwa Airtel Tanzania Plc imetoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 500 huku wafanyakazi wa kigeni wakiwa saba tu na kupitia kampuni hiyo, Watanzania 350,000 wamejiajiri kwa kuuza huduma za kampuni ya Airtel Tanzania Plc kama vile kuuza vocha, mawakala wa Airtel Money hivyo kuchangia maendeleo ya uchumi kwa kulipa ushuru kwa Serikali

 

Airtel pia imetoa  2.3 bilioni kwenye ujenzi wa Hosptili mkoani Dodoma na kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (VETA) kuzindua elimu kwa mtandao kupitia Program Tumishi (App) ya VSOMO ambapo  wanafunzi zaidi ya 500 wamehitimu.

 No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.