AIRTEL MONEY YAGAWA GAWIO LA SH.BILIONI 3.6 KWA WATEJA NCHINI TANZANIA
Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kutangaza kuanza kugawa Tzs 3.6 bilioni kama gawio la faida kwa wateja na mawakala wa Airtel ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo.
Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma ya Airtel Money Jumatano ya Septemba 9 2020, imetangaza kuanza kugawa Sh 3.6 bilioni kama gawio la faida kwa wateja ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari wakati wa kutangaza hatua hiyo ya kugawa gawio la faida kwa wateja wa Airtel Money Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema kuwa faida hiyo itagaiwa kwa wateja wote wa Airtel Money pamoja na mawakala nchini ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kwa kipindi cha Oktoba 2019 mpaka Machi 2020.
Nchunda alieleza kuwa Airtel imekuwa ikigawa gawio hilo la faida kwa wateja wake wa Airtel Money pamoja na mawakala tangu 2015. Faida hii anaipata mteja yeyote wa Airtel kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti yake yaani salio la Airtel Money. Gawio hili la faida limekuwa likitolewa na Airtel tangu mwaka 2015 ambapo hadi Septemba 9 jumla ya Shilingi bilioni 24 zitakuwa zimegawiwa kwa mgawanyo tofauti tofauti na kuwafikia wateja pamoja na mawakala wote nchini Tanzania Nchunda.
Mteja anaweza kutumia faida hiyo kwa matumizi mbali mbali ikiwemo kununua bando, muda wa maongezi, kulipia bili kama vile Dawasco, LUKU, Dstv, ama anaweza akatoa fedha hizo kwa matumizi ya kawaida au kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Beatrice Singano alisema kuwa kila mteja wa Airtel Money pamoja na mawakala watapata faida yao kupitia akaunti zao za Airtel Money.
Huduma za Airtel Money hupatikana pia kupitia program tumishi ya Airtel Money kwenye duka la mtandaoni la Play Store au App Store
Huduma ya Airtel Money imeunganisha na huduma za biashara zaidi ya 400 pamoja na benki zaidi ya 30 ambapo mteja anaweza kufanya malipo au miamala akiwa popote pale kwa kutumia simu. Vile vile wateja wanaweza kulipia huduma na bili mbali mbali kama vile TRA, LUKU, malipo ya serikali na zingine nyingi.
Post a Comment