MTANGAZAJI

RUKSA KUUZA MADINI YA BATI NJE YA NCHI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0hYFWChB6bknZ2kbr331sEeU-jG4npmM5Bmt0HMQa6bibGmWq2UDVt__4CjeaOhXg5e2Zx-q4xES-i6UZcC2UxBtmzYYD_oy0j0HkZCgn_U1lOmwwA4WagL0jF6QJvxUHE2zdaMFDeLMz/s1080/IMG-20200810-WA0030.jpg
WAZIRI wa Madini Doto Biteko akitoa kwenye ukumbi wa mikutano wa soko la madini ya bati(TIN) Kyerwa mara baada ya kumaliza mkutano na wachimbaji wa madini hayo

Serikali ya Tanzania imewaruhusu  wafanyabiashara wa Madini ya Bati kuyasafirisha madini yaliyoongezwa thamani kwenda kuuzwa nje ya nchi ili yauzwe kwa bei nzuri na wachimbaji kufaidika.

 Taarifa hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Madini nchini Tanzana Doto Biteko wakati wa  ziara yake ya kikazi wilayani Kyerwa Mkoa wa Kagera ambapo alizungumza na wachimbaji pamoja na wafanyabiashara wa  Madini ya Bati (TIN) kwenye  ukumbi wa mikutano wa soko la madini ya bati mara baada ya kumaliza mkutano na wachimbaji wa madini hayo.

Waziri Biteko pia  amewataka wachimbaji wa Madini ya Bati kurejea kazini na kuachana na vitendo vya kutorosha madini hayo na badala  yake wayapeleke sokoni.

 Amewataka wachimbaji hao kupendana, kuthaminiana na kuachana na mambo ya majungu ili kujikita katika kuongeza tija kwenye shughuli yao ya uchimbaji madini.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashidi Mwaimu alimpongeza Waziri wa Madini, kwa kazi nzuri anazozifanya na kuwataka wachimbaji wa Madini ya Bati kutumia fursa hiyo kueleza changamoto zao mbele ya Waziri.

Nae, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Madini ya Tin wilayani Kyerwa Osward Inyasi, kwa niaba ya wachimbaji wenzake alieleza kuwa wachimbaji wa madini ya Tin bado wanashida ya wanunuzi wa madini yao kwani hadi sasa wana zaidi ya tani 20 zimewekwa stoo baada ya kukosa wanunuzi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.