MTANGAZAJI

MCH GLENWARD ALEXANDER BRYANT ACHAGULIWA KUONGOZA KANISA LA WAADVENTSTA AMERIKA YA KASKAZINI



Kikao cha Kamati Kuu ya Konferensi Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani  kilichofanyika Juni 9,2020 kilimempitisha Mch Glenward Alexander Bryant (Pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Divisheni ya Amerika ya Kaskazini  katika hilo (NAD) akichukua nafasi ya Mch Daniel R.Jackson ambaye alidumu katika nafasi hiyo toka Juni 2010 na kustaafu Juni mosi mwaka huu.

Kwa kura 153 kati ya kura 158 zilizopigwa na Kamati hiyo iliyofanya kikao  chake kwa njia ya mtandao  ili kupitia na kupigia kura mapendekezo yaliyotolewa na Kamati Kuu ya Divisheni ya Amerika ya Kaskazini ya Kanisa la Marekan la Waadventista wa Sabato kuhusu jina la Mchungaji  Bryant kuwa  Mwenyekiti mpya wa Divisheni hiyo,kamati ilithibitisha mapendekezo hayo kwa kura za NDIO 153 na HAPANA kura 5 tu.

Kabla ya Mapendekezo hayo Mch. Bryant  ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Pili mwenye asili ya Afrika kuchaguliwa  toka mwaka 1979  katika Divisheni hiyo iliyoanzwa mwaka 1913  alikuwa ni Katibu Mkuu.

Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuwa Divisheni ya Amerika ya Kaskazini ya Kanisa la Waadventista wa Sabato inayohusisha nchi ya Marekani,Canada na Visiwa vya Guam ina idadi ya makanisa 5,606 yenye waumini 
1,257,913

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.