MASHINDANO YA USOMAJI WA BIBLIA KWA VIJANA WA KIADVENTISTA YAFANYIKA HOUSTON MAREKANI
Jumla ya timu 10 za Watafuta Njia kati ya Arobaini toka kwa
Makanisa ya Waadvetista wa Sabato katika jiji la Houston,Marekani
zimefanikiwa kuingia katika hatua ya pili ya Mashindano ya Uzoefu wa
Usomaji wa Biblia yanayoendeshwa na idara ya huduma za Vijana kwa
vilabu vya watafuta njia vya Divisheni ya Kaskazini mwa Amerika (NAD)
mwaka huu.
Hatua hiyo ya kwanza ambayo
imefanyika katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la Nations of Praise
iliwakutanisha watafuta njia 255 kwa kujibu maswali 90 toka katika
vitabu vya Ezira,Nehemia,Amosi,Yona,Mika na Hosea ambapo iliwachukua
takribani saa 6 kukamilika kwa zoezi hilo na kisha kutangazwa washindi
huku Timu tano za Kanisa la Waadventista wa Sabato la Houston
International zikiiongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa kila timu.
Mashindano
ya Uzoefu wa Usomaji wa Biblia kwa watafuta Njia yanaendeshwa na NAD
ambapo kila timu ya vijana sita wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16
husoma Biblia,na kisha kufanya mtihani kutokana na vitabu vya Biblia
vilivyopangwa kwa mwaka husika wakiwa chini ya walimu waliopangwa na
makanisa mahalia.
Asilimia za upangaji wa
matokeo hutokana na majibu ya maswali yaliyoulizwa ambapo timu inayopata
asilimia 90 hushika nafasi ya kwanza,asilimia 80 nafasi ya pili na
nafasi ya tatu ni iliyopata asilimia 70 ya majibu ya maswali.
Post a Comment