MTANGAZAJI

WATANZANIA WAHIMIZWA KUJENGA UTARATIBU WA KUPIMA AFYA ZAO

 
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa tiba ya bure kutoka kwa madaktari na wauguzi kutoka nchi Mbalimbali walioweka kambi ya uchunguzi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza

Wananchi nchini Tanzania  wametakiwa kujenga utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini aina ya magonjwa wanayokabiliana nayo ili kuweza kuanza tiba mapema kabla ya ugonjwa kukithiri.

Hayo yamebainishwa na wakati wa uzinduzi wa tiba ya bure kutoka kwa madaktari na wauguzi kutoka nchi mbalimbali walioweka kambi ya uchunguzi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza.

Jopo hilo la wahudumu wa afya ambalo linaratibiwa na taasisi ya Head INC yenye maskani yake nchini Marekani lipo wilayani humo kwa ajili ya kuchunguza afya za wakazi wa wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mratibu wa Head Inc (Diaspora) Asha Nyanganji alisema kwamba lengo la ziara hiyo kutoa elimu na huduma za afya wataalamu waliokuwa wanafanyakazi na wataalamu wa Tanzania  na hivyo kubadilisha uzoefu.

Asha aliwataka watanzania kuweka utaratibu wa kuangalia afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini magonjwa yanayowasumbua ili kuweza kupata matibabu mapema badala ya kusubiri mpaka wanapozidiwa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.