TUZO YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI YAKABIDHIWA KWA WAZIRI KIGWANGALLA
Kamishna
wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi
akikabidhi tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ,Jenerali Mstaafu
,George Waitara ili aikabidhi kwa Waziri ,Dkt Kigwangalla
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ,Jenerali Mstaafu ,George Waitara akikabidhi tuzo
iliyotolewa kwa Hidahi ya Taifa ya Serengeti kwa Waziri wa Maliasili na
Utalii ,Dkt Kigwangalla wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika
viwanja vya TGT jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Jenerali Mstaafu wa Jeshi ,George
Waitara amekabidhi kwa Waziri wa Utalii na Maliasili Dkt Khamis Kigwangalah tuzo iliyoshinda
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kutangazwa hifadhi bora barani Afrika.
Tuzo hiyo iliyotolewa na taasisi ya World Travel Award (WTA)
Juni Mosi nchini Mauritius baada ya Hifadhi ya Serengeti kuwa na sifa za
kipekee miongoni mwao ikiwa ni idadi kubwa ya wanyama wahamao,wanyama walao
nyama na uwepo wa ukanda mrefu wenye
wanyama wengi imepangwa kukabidhiwa kwa raisi Dkt John Magufuli .
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo hiyo kwa
Waziri Kigwangala,hafla iliyofanyika katika viwanja vya TGT yanapofanyika
maonesho ya Utalii ya Karibu/Kili fair
,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugnzi TANAPA ,George Waitara amesema ushindi
wa Hifadhi ya Serengeti kuwa Hifadhi Bora ni ushindi wa Watanzania wote.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf
Mkenda amesema tuzo hiyo imepatikana baada ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
kushindanishwa na Hifadhi nyingine kubwa tano barani Afrika kwa watalii kupiga
kura.
Post a Comment