MTANGAZAJI

WAZIRI MKUU WA TANZANIA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA WAADVENTISTA LA MAGOMENI DAR ES SALAAM


Waziri Mkuu Kassim Majariwa akihutubia waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Magomeni Mwembechai


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mch Mark Walwa Malekana ambaye ni Mwenyekiti wa Unioni ya Kusini katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania.



Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameshiriki katika Sabato maalum ya kuadhimisha miaka 100 ya Idara ya Huduma za Familia ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni, katika Kanisa la Magomeni Mwembechai Jijini Dar es salaam Mei 11,2019.

Katika ibada hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Viongozi wa Kanisa hilo katika Unioni ya Kusini mwa Tanzania akiwemo Mwenyekiti wake Mch Mark Walwa Malekana,Waziri Mkuu amechangia mifuko 300 ya saruji na fedha taslimu shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Magomeni Mwembechai.


 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.