MTANGAZAJI

WANAFUNZI WA KIADVENTISTA WAKUSANYA MICHANGO KUSAIDIA WAISLAMU



Kikundi cha wanafunzi wa shule ya sekondari ya New Zealand kinakusanya michango ya fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa shambulio la kupigwa risasi kwa waumini wa dini ya kiislamu katika msikiti wa Christchurch machi 15 mwaka huu nchini humo..

Amelia Tyrrell, mwenye umri wa miaka 17, na viongozi wenzake wa shule ya sekondari ya  Kiadventista ya Chuo cha  Longburn  wamekusanya mchango kutoka kwa wanafunzi wenzao  na kutuma kwa waathirika wa shambulio hilo linaloelezwa kuwa la kigaidi.
Mshambuliaji mwenye itikadi kali za ubaguzi wa rangi aliwaua watu 50 katika misikiti miwili Ijumaa iliyopita.
Mkuu wa Shule Brendan van Oostveen amesema  Jumatano ya  Machi 20, kila mwanafunzi na wafanyakazi wa chuo wa shule ya Longburn walivaa maua kichwani ,shingoni na mengine kuyashika mkononi huku wakikusanya michango kwa ajili ya kutoa misaada kwa wahanga wa tukio hilo ambao miongoni mwao ni wakimbizi waliofika katika eneo hilo miezi 18 iliyopita.
Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Sophie Pigott ,mwenye umri wa miaka saba ameeleza kuwa wameguswa na tukio hilo  huku  akifafanua kuwa amani upendo heshima ni mambo yanayothaminiwa na waislamu na wakristo kwa raia wa New Zealand.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.