MTANGAZAJI

ADRA YATOA MISAADA YA KIUTU NCHINI MSUMBIJI NA ZIMBABWE






Kimbunga Idai kilichoikumba Msumbiji, Malawi, na Zimbabwe Machi 15-17 mwaka huu  na kuacha maelfu ya watu wakiyahama makazi yao huku ripoti za awali zikieleza kuwa watu 84 walithibitishwa kupoteza maisha nchini Msumbiji. 

Kwa mujibu wa Rais wa Msumbiji, Felipe Nyusi vifo vya watu viliongezeka na kufikia takribani watu 1,000 nchini Msumbiji pekee huku zaidi ya watu milioni 1.7 toka nchi tatu wakiathiliwa  baada ya kimbunga hicho.
 
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alitangaza dharura ya kitaifa baada ya dhoruba kali iliyoikumba nchi hiyo na kuua watu wapatao 98. 


Madaraja na barabara zimeharibiwa , nyumba zaidi ya 100 zilianguka, na zaidi ya watu 70 waliripotiwa kukosa makazi. Jitihada zinazoendelea za uokoaji ziliendelea nchini Zimbabwe na maeneo yote yaliyoathirika  nchini Msumbiji na Malawi.

Shirika la Waadventista  linalojihusisha na misaada wakati wa Majanga (ADRA) limetoa misaada ya dharula nchini Zimbabwe, kusaidia kaya 650 kwa chakula na nguo huku kukiwa na mipango zaidi ya kutoa msaada mchini  Msumbiji na Malawi.


Machi 18 mwaka huu  ADRA ilisaidia makazi  ya watu 3,000 katika jiji la Beira nchini Msumbiji Msumbiji huku ikiendelea kuratibu mipango mbalimbali ya utoaji wa misaada kwa kushirikiana na taasis zingine za kimataifa.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.