Jengo
kubwa kabisa duniani (sio refu, bali kubwa) ni karakana ya kuunganisha
ndege za Boeing 747, 767, 777, na 787 liko Washington State nchini Marekani.
Jengo hili lina ukubwa wa futi za
mraba zaidi ya milioni 472.
Jengo hili ni kubwa kiasi kwamba kabla
halijawekewa mfumo maalum wa kuzungusha hewa, lilikuwa likitengeneza
mawingu ndani ya jengo.
Ni hapa ambapo ndege za Boeing zimekuwa
zikiunganishwa tangu enzi za vita ya pili ya dunia.
Baadhi ya mambo
muhimu kujua ni....
1: Jengo hili liko kwenye eneo la ekari 98.7, lina
wafanyakazi 30,000 ambamo humo ni kama jiji. Kuna migahawa dazeni
kadhaa. Huduma za kulea watoto (child care), ATMs na kadhalika.
2: Lina
njia za chini ya ardhi kwa watembea kwa miguu zenye urefu wa maili 2.33
kuwawezesha wafanyakazi 'kusafiri' toka upande mmoja wa jengo hadi
mwingine.
3: Lina zaidi ya taa milioni moja.
4: Lina zaidi ya baiskeli
na guta 1,300 kuwawezesha wafanyakazi kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyingine
Post a Comment