AJALI YA NDEGE YA ETHIOPIA:MWADVENTISTA AKATAA KUZIKA UDONGO ULIOKUSANYWA KATIKA ENEO LA AJALI
Raia wa Kenya aliyewapoteza ndugu
watano katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia amekataa kuzika
udongo uliokusanywa kutoka katika eneo la ajali.
Paul Njoroge amepoteza mke,mtoto
wa kike,na wajuu watatu ambao walikuwa abiria katika ndege ya Boeng 737 Max-8 iliyoanguka jumapili ya Machi
10 na kuua abiria 149 na wafanyakazi wanane.
Jumatano Machi 20 mwaka huu katika huduma ya
maombi iliyofanyika huko Bahati ,Nakuru,Njoroge ambaye ni Mwadventista wa
Sabato amesema amepokea kwa maumivu na masikitiko tukio laa kuondokewa na ndugu na kwa sasa anasubiri matokeo
ya vipimo vya vinasaba (DNA) japo muda uliotolewa ni mrefu .
Ameeleza kuwa kipindi cha miezi
sita kilichotolewa na serikali kwa ajili ya kufanya upembuzi wa vipimo vya
vinasaba kutoka katika vipande 5000 vya mabaki ya miili iliyokusanywa kutoka
katika eneo la ajali ni kipindi kirefu hivyo atafarijika tu kwa huduma ya maombi
ya faraja kwa ndugu na jamaa ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo ambayo
itafanyika Machi 29 mwaka nchini humo.
Njoroge ambaye amepoteza ndugu hao watano amesema
imani ya dini yake hairuhusu kuzika udongo uliokusanywa kutoka Bishoftu
kilomita 60 kusini mwa mji wa Addis Ababa ambako mamlaka zinafanya uchunguzi wa
kutambua miili ya waliopoteza maisha.
“Hili ni jambo kubwa
kwangu,linaumiza sana,lakini nafikiri hakuna ninachoweza kufanya bali kulipokea
na kulikubali na acha watu waendelee na maisha”amesema Njoroge.
Shirika la ndege la Ethiopia
limesema litalipa fidia kwa familia zilizopoteza wapenda wao kutokana na ajali
hiyo ya ndege.
Post a Comment