MTANGAZAJI

VIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO TANZANIA WATEMBELEA KULIKOTOKEA MAUJI YA MUUMINI


Dkt Godwin Ole Lekundayo akitoa neno la Faraja


Katibu wa NTUC Mch David Makoye
Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato katika Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania (NTUC) Mwenyekiti  Dkt Godwin Ole Lekundayo na Katibu Mch David Makoye walitembelea katika Kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye kijiji cha Kazikazi,Itigi mkoani Singida kwa ajili ya kuwafariji waumini wa Kanisa hilo kutokana na kifo cha Isaka Petro ambaye inaelezwa na jeshi la polisi kuwa alifariki kwa kupigwa risasi Sabato ya Februari 2,mwaka huu saa 8:20 kanisani hapo
 Jeshi la Polisi linawashikilia watu saba kwa mahojiano kutokana na mauaji hayo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Pius Shija Luhende.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.