MTANGAZAJI

MTENDE FAMILY SINGERS TOKA 2016 HADI NYUMBANI HATIMAYE 2019 (+VIDEO)
Kama umekuwa ukifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya Mkutano wa Nyumbani Hatimaye 2019 ulioanza Februari 2 mwaka huu unaorushwa toka Kinyerezi jijini Dar es salaam Tanzania kila siku saa 12 jioni kwa saa za Tanzania mbashara kwa Morning Star Radio na Hope Channel Tanzania utakuwa umeusikia wimbo wa Mkutano  "Hatimaye Tutafika Nyumbani" unaoimbwa na watu wote walioko Kinyerezi na waofutilia mkutano huo duniani kote ukiongozwa waimbaji wa Mtende Family.

Mtende ni jina la kikundi cha uimbaji kinachopatikana katika Kanisa la Waadvestista wa Sabato Kinyerezi, Dar es salaam, Tanzania. Kikundi hiki kilianzishwa Septemba 2016 Septemba kikiwa na waimbaji wanne. Waimbaji hawa ni Happy Wikedzi, Twininge Michael Mwaitete, Alphonce Magori Bulahya na Marwa Magori Nyamhanga.
Mwaka 2017 waimbaji watatu walijiunga na kufanya idadi ya waimbaji saba , waimbaji wa kiume watatu  na waimbaji wakike wanne.
  • Kwa nini Mtende? 
Marwa Magori anaeleza kuwa jina hili linatokana  na sifa njema za mmea huu wa mtende. Mtende ni mmea unaopatikana katika uoto wa jangwa. Mmea huu uvumilia ukame na joto la jangwani. Ni mmea wenye sifa nyingi sana ambazo kila mmoja wetu anatakiwa kujifunza mambo mengi ya kiroho, kiakili na hata kimwili.
  • Mpaka sasa Mtende wamepata mafanikio yapi?
Kikundi kimefanikiwa kutoa santuri ya sauti namba moja  yenye nyimbo nane iliyotoka  mwaka 2017 na sasa wapo kwenye mchakato wa kutoa santuri mwonekano kabla ya mwisho wa mwaka huu.
  • Ilikuwa je Wimbo wa Mkutano -Hatimaye Tutafika Nyumbani?
Magori anaeleza kuwa huu ni wimbo unaoendana na kichwa kikuu cha Mkutano wa Nyumbani Hatimaye,Wimbo huu unatia moyo na hamu ya kuyafikiria makazi tuliyoandaliwa na BWANA wetu. Maana Yeye alisema ``Msifadhike mioyoni mwenu…..nitakuja niwachukue kwangu ili nilipo mimi nanyi mwepo ( Yohana 14:1-3).
Mtunzi wa wimbo huu ni Mgini Kweba mwalimu wa Kwaya ya Waadventista wa Sabato Magomeni Mwembechai, ambaye amekuwa mbaraka wa kushangaza kwa kazi ya Mungu kupitia uimbaji wa nyimbo za Injili katika kanisa hilo.
Waimbaji wanaunda Mtende Family kwa sasa ni Grace Bilshani Otieno,Twininge Michael Mwaitete,Happy Ibrahim Wikedzi,Sara Kapis Obango,Alphonce Magori Bulahya,Amos Manane Amenya na Marwa Magori Nyamhanga.
Mtende wanapatikana kwa   mtendesingers@gmail.com 
na kwa  ya Youtube kwa  Mtende Singers

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.