MTANGAZAJI

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AAGIZA ZAHANATI YA WAADVENTISTA WA SABATO IPANDISHWE HADHI

-->

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe akipokelewa na Mwenyekiti wa Jimbo Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT) Mch Joseph Mngwabi,katikati ni Katibu Mkuu wa Jimbo hilo  Mch Francis Katengu

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh. Daktari Kebwe Steven Kebwe amefanya ziara ya ukaguzi katika Zahanati ya  Misufini inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Jimbo la Mashariki Kati mwa Tanzania (ECT)  na kuridhishwa na huduma zitolewazo na kituo hicho na kuagiza zahanati hiyo ipandishwe hadi na kuwa kituo cha Afya baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.

Dkt Kebwe Steven Kebwe ambaye ameambatana na Mkurugengi wa wa manispaa ya Morogoro pamoja na Kaimu Daktari Mkuu wa mkoa wa Morogoro amelishukuru kanisa la Waadventista kwa kushiriki kwake katika kutoa huduma za afya kwa wananchi kupitia Zahanati hiyo ambayo ndio dhamira kuu ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.