NYARUGUSU:KWAYA YA VIJANA NYARUGUSU WAREKODI VIDEO YAO MPYA NA JCB STUDIOZ YA JIJINI DAR ES SALAAM
Hatimaye Kwaya ya Vijana ya Nyarugusu toka Geita Tanzania imefanikiwa kurekodi toleo la kwanza la Santuri Mwonekano lenye nyimbo tisa iliyoongozwa na Mtayarishaji wa Video toka JCB Studioz za jijini Dar es salaam,Moses Romeo
Akizungumza na blog hii toka Nyarugusu,Moses Romeo amesema video hiyo iliyopewa jina la Amri Kumi imehusisha maeneo ya mbalimbali ya Nyarugusu na mjini Geita kama yanavyoonekana kwenye picha.
Kwaya ya Vijana ya Nyarugusu yenye matoleo manne ya audio ilionesha umahiri katika uimbaji wa Nyimbo za Injili kwenye Mkutano wa Ushindi Hatimaye 2017 uliokuwa ukirushwa na mubashara toka Mabatini Mwanza na Morning Star Radio,Morning Star Tv na Star Religion.
Miongoni mw Nyimbo za kwaya hiyo ni Jerusalemi,Leta Roho na Kornelio zote toka katika toleo lao namba tatu la audio.
Post a Comment