MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:JENGO LA HOLIDAY INN LAWA KIVUTIO KWA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI


Sonda ya Dihlu waliokuwa wakirekodi video yao katika jengo hiloFamily Music wakirekodi video yao juu ya jengo la Holiday Inn Dar es salaam


Jengo la refu la Holiday Inn la jijini Dar es salaam limeanza kupata umaarufu kwa waimbaji wa nyimbo za Injili kurekodi nyimbo zao juu ya jengo hilo.

Imeelezwa na waimbaji pamoja na watayarishaji wa video kuwa mandhari ya jengo hilo inasaidia kupata video bora na zinazovutia kwa watazamaji.

Miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za Injili waliotumia jengo hilo kurekodi video zao ni Sonda ya Dihlu katika santuri yao mwonekano iliyorekodiwa na HomeTown Records ambayo imeshatoka,Wengine ni Family Music katika video yao mpya itakayotoka hivi karibuni iliyorekodiwa na JCB Studioz.

Mmoja wa wasimamizi wa jengo hilo ambaye hakutaka jina lake amesema kuna maombi mengi sasa toka kwa waimbaji kutaka kurekodi video zao juu ya jengo hilo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.