TUKUYU: KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LAVAMIWA NA KUCHIMBULIWA SHIMO KWA MADAI KUNA MADINI
Watu
wasiofahamika, wamevamia na kuchimba shimo kubwa ndani ya Kanisa la
Waadventista Wa Sabato katika kijiji cha Masoko kilichopo wilayani Rungwe
nje kidogo ya mji wa Tukuyu.
Watu hao inasadikika wanaeneza uvumi kuwa
kuna vito au Rupia( pesa ya zamani ya wajerumani). Ofisi ya madini
imekanusa kuwepo kwa madini yeyote katika eno hilo huku jeshi la Polisi
likiahidi kuwatafuta wote waliohusika na uharibifu huo.
Kanisa hilo ndilo la kwanza katika jimbo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania lilijengwa mwaka 1932,jengo la awali lilibomolewa na juu yake kujengwa kanisa jingine mwaka 1967.
Post a Comment