MTANGAZAJI

VIDEO MPYA INAYOMTAMBULISHA SUZAN MALALE TOKA TANZANIA

Mwimbaji anaitwa Suzan Malale toka Mbagala jijini Dar es salaam ambaye kwa kweli huenda kitambulisho chake kinaweza kukushangaza zaidi hasa ukimuona alivyo mpole lakini sauti yake haiendani na upole wake ama unaweza usiamini kama anaweza kuimba.

Suzan Malale alianza kuimba toka akiwa anasoma sekondari huko Arusha nchini Tanzania na ndiye mwanzilishi wa kundi la Joyful Voices ambalo pia mwimbaji Angel Magoti aliwahi kuimba nalo ambalo lina matoleo mawili sasa.

Suzan Malale sasa tayari ameshatoa santuri yake mwonekano ya kwanza yenye nyimbo zinazojaribu kuelezea maisha yake halisi aliyoyapitia.
Angalia video ya miongoni mwa nyimbo zake hapa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.