UCHAGUZI WA RAIS WA MAREKANI MWAKA HUU WAELEZWA KUTUMIA PESA NYINGI ZAIDI KULIKO CHAGUZI ZILIZOPITA
Haijalishi nchi yaweza kuwa tajiri ama maskini hapa duniani, kuna mambo mawili ambayo yanaelezwa kuwa yamekuwa yakitumia gharama kubwa katika mataifa mbalimbali dunia,mambo hayo ni masuala ya vita na uchaguzi.
Kwa mujibu wa mtandao wa gobankingrates.com,uchaguzi uliomalizika hivi karibuni nchini Marekani katika kumtafuta rais wa nchi hiyo imeelezwa kuwa ni uchaguzi uliotumia gharama kubwa kuliko chaguzi zilizopita,ambapo kwa mujibu wa mtandao huo hadi kufikia Oktoba 25,2016 jumla ya dola za kimarekani Bilioni 6.6 zilikuwa zimeshatumika,Ambapo waliokuwa wapinzani wakuu katika kinyang'anyiro hicho Trump na Bi Clinton walikuwa wameshatumia dola bilioni 1.13 kwa shughuri za kiofisi ukilinganisha na dola milioni 913 zilizotumika kwenye uchaguzi mwaka 2012.
Kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg Donald Trump alitegemea sana katika utajiri wake na kutoka kwa wadau wake,hadi Oktoba 19,2016 Trump alikuwa ameshachangia pesa zake mwenyewe kiasi cha dola milioni 56.2 na akatumia jumla ya dola milioni 429.5.
Bi Clinton aliweza kuchangisha kiasi cha dola bilioni 1.06 na akawa ametumia dola milioni 897 huku akitumia dola milioni 125.1 katika vyombo vya habari akimzidi Trump kwa kiasi cha dola milioni 30.4.
Post a Comment